Ni wapi mwanamke anabaki wapi baada ya ile talaka ya tatu?

Swali: Mwanaume akimtaliki mke wake mara tatu. Hivi sasa yuko katika eda. Je, abaki kwenye nyumba hiohio au atoke?

Jibu: Abaki kwenye nyumba hiohio, lakini avae Hijaab mbele yake na ajilinde nae:

لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِن بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُجْنَ

“Msiwatowe katika nyumba zao na wala wao wasitoke… “[1]

Abaki kwake na khaswa khaswa ikiwa ameshazaa nae watoto.

[1] 65:01

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ighaathat-il-Lahfaan (59) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-29-01-1438_0.mp3
  • Imechapishwa: 03/11/2017