Hadiyth hii kubwa ambapo Mu´aadh anabainisha yale Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyomtuma kwa watu wa Yemen kuna faida zifuatazo:

Uwajibu wa kuwatuma walinganizi wanaolingania katika dini ya Allaah. Hili ni jukumu la mtawala. Ni wajibu kwa mtawala wa waislamu awatume walinganizi wa Allaah katika kila mahali. Kila mahali ambapo kunahitajika Da´wah basi ni wajibu kwa mtawala wa waislamu amwagize mtu ambaye atawalingania watu katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall). Huu ni uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwatuma wajumbe ili walinganie watu katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/502)
  • Imechapishwa: 10/09/2025