Swali: Vipi mwanaume kutazama picha za wanaume katika TV?

Jibu: TV yenyewe ina khatari. Ni wajibu kutahadhari nayo. Ni wajibu kujitenga mbali na shari yake na maharibifu yake. Isipokuwa kutazama mihadhara na matendo mengine yanayowafaa waislamu. Kuhusu yeye mwanamke atazame mtazamo usiokuwa wa shahawa wala mashaka. Ikiwa ni mtazamo wa kawaida haidhuru.

Swali: Vipi ikiwa TV iko chini ya uangalizi ambapo watu wanatazama vipindi vya kielimu?

Jibu. Kwa hali yoyote hapana vibaya ikiwa mwanaume anaweza kufanya hivo. Hata hivyo TV ni khatari na hivyo ni lazima kujihadhari nayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23916/حكم-نظر-المراة-الى-صورة-في-التلفاز
  • Imechapishwa: 31/05/2024