Ni wajibu kulipa deni la watu kabla ya kufanya ´Umrah?

Swali: Je, inamlazimu mtu kulipa deni kabla ya kufanya ´Umrah?

Jibu: Kama ana uwezo wa kulilipa deni, basi afanye ´Umrah. Kama hana uwezo, aanze na deni kwa sababu deni ni wajibu na ´Umrah inapendeza. Mwenye kuwa na madeni, gharama za ´Umrah aziweke kwa baadhi ya wadai wake.

Mwanafunzi: Ikiwa mwenye kudai atampa muda?

Ibn Baaz: Ikiwa ni mwenye kudai aliye na mipaka, mtu mmoja au wawili, hakuna tatizo.

Mwanafunzi: Hukumu hiyohiyo inahusu hajj?

Ibn Baaz: Hukumu hiyohiyo inahusu hajj.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30886/هل-يجب-قضاء-الدين-قبل-الحج-والعمرة
  • Imechapishwa: 14/09/2025