Ni vipi nitajua ni wepi walio katika haki na wepi walio katika batili?

Swali: Ikiwa ndio nimeanza kushikamana na msimamo ni vipi nitajua ni mlinganizi yupi anayelingania katika haki na ni yupi anayelingania katika fitini?

Jibu: Waislamu wako na wanachuoni ambao ni wakweli na wana Ikhlaasw kama mfano wa Shaykh Ibn Baaz, Shaykh Ibn ´Uthaymiyn, Shaykh Fawzaan na wanachuoni wengineo katika kila mji miongoni mwa miji. Jamii ambayo imeshikamana na Qur-aan na Sunnah wasomewe [vitabu na maneno yao] na watakwe ushauri katika mambo ya tofauti. Halafu Wasomee kitabu “al-Milal”. Soma kuhusiana na mambo haya basi utapata kutambua mambo mengi. Ikiwa wewe ni mwanafunzi ambaye ni imara basi unaweza kutambua mambo mengi kwa kusoma wewe mwenyewe kisha kumtaka msaada Allaah kisha kuwataka msaada wanachuoni, wakweli na wenye fadhila. Vilevile kwa kurejea kwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Unatakiwa kusoma:

اللَّهُمَّ رَبَّ جِبْرِيلَ وَمِيكَالَ وَإِسْرَافِيلَ فَاطِرَ السَّمَواتِ والأَرْضِ عَالِمَ الْغَيْبِ والشَّهَادَةِ أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادك فِيما كانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بإِذْنِكَ إِنَّكَ تَهْدِي مَنْ تَشَاءُ إِلى صِرَاطٍ مُسْتَقِيم

“Ee Allaah! Mola wa Jibriyl, Mikaaiyl na Israafiyl! Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ambaye ni Mjuzi wa mambo yenye kujificha na yalio ya wazi! [Siku moja] utahukumu baina ya waja Wako katika mambo ambayo walikuwa wakitafautiana! Niongoze mimi katika haki katika yale waliotafautiana kwa idhini Yako – Hakika Wewe unamuongoza umtakae katika njia ilionyoka.”

Yule ambaye nia yake itakuwa haki basi ataifikia – Allaah akitaka. Atakayemtakasia nia Allaah na akawa mkweli basi ataitambua haki ni ipi na batili ni ipi – Allaah akitaka – baada ya kutumia sababu kama hizi.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda: Ujuw al-I´tiswaam bil-Kitaab was-Sunnah http://rabee.net/ar/questions.php?cat=29&id=294
  • Imechapishwa: 14/04/2018