Ni vipi namna ya kuyaswalia makaburi mawili baada ya kuzikwa?


Swali: Makaburini kuna makaburi mawili yaliyo karibu. Ni vipi mtu atayaswalia baada ya kuzikwa? Je, kila limoja liswaliwe kivyake au mtu anuie kuyaswalia yote mawili kwa wakati mmoja?

Jibu: Ikiwa makaburi hayo mawili yako mbele ya mwenye kuswali ayaswalie swalah moja. Ikiwa kila limoja liko sehemu yake, basi kila limoja aliswalie swalah yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/160)
  • Imechapishwa: 15/09/2021