Ni vipi kutathibitishwa ´Aliy kukingwa na kukosea?

Jambo la tatu: Wacha tukadirie kuwa kweli ´Aliy amekingwa na kukosea. Ikiwa Shiy´ah wametofautiana na kutawanyika kiasi hiki, mtu anaweza kujiuliza ni maneno yepi yanayonasibishwa kwake ni ya kweli na yepi yasiyokuwa ya kweli. Kila mmoja anadai kwamba wameyapokea kutoka kwa wale ambao wamekingwa na kukosea. Shiy´ah hawana cheni za wapokezi zilizoungana zilizo na wanaume wanaotambulika kama zilivyo cheni za wapokezi wa Ahl-us-Sunnah ili mtu aweze kutazama cheni hizo na uadilifu wa wanaume hao. Bali wana nukuu zilizokatika kutoka katika kakundi ka watu ambao wanajulikana kwa kusema uongo sana na kujigonga katika yale wanayopokea. Hivi kweli mwenye akili ataamini hilo?

Ikiwa watadai kuwa haya wameyapokea kwa mapokezi mengi (Tawaatur), basi madai yao yanakutana na madai ya wengine ambao nao wanadai kuwa wamepokea kupitia njia nyingi. Hivyo kutakuwa hakuna tofauti yoyote kati ya madai hayo mawili.

Haya yanapata kubainisha kwamba madhehebu ya Shiy´ah hayakuchukuliwa kutoka kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) ikiwa tutasema kweli kwamba amekingwa na kukosea. Madai hayo yanayosema kwamba ´Aliy amekingwa na kukosea ni kama madai ya manaswara wanaposema kwamba ´Iysaa ndiye mungu pamoja na kwamba mafunzo yao hawakuyachukua kutoka kwake.

Jambo la nne: Shiy´ah wanahitajia tangulizi mbili:

1- Mtu ambaye wanamnasibishia madhehebu ya maimamu anatakiwa kuwa amekingwa na kukosea.

2- Nukuu hiyo ni lazima ithibiti kwa imamu huyo aliyenukuliwa kutoka kwake.

Tangulizi zote mbili ni batili. ´Iysaa sio mungu. Lakini yale yanayosemwa na manaswara sio maneno yake.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (4-18/19)
  • Imechapishwa: 08/12/2018