Ni swalah zipi ambazo watu wanafaa kukusanya msikitini wakati wa mvua?

Swali 284: Nilimuuliza kuhusu ambaye anakusanya kati ya ´Ishaa  na Maghrib na kama jambo la kukusanya ni maalum kwa ajili ya swalah hizo mbili?

Jibu: Kuna maoni yanayosema hivo, kutokana na kwamba uzito unakuwa mkubwa zaidi. Sahihi ni kwamba inahusu vilevile Dhuhr na ´Aswr.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 102
  • Imechapishwa: 17/05/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´