Ni sawa baadhi ya nyakati kuwaswalisha familia mkusanyiko

Swali: Imaam ash-Shaafi´iy kutumia dalili kwa Hadiyth hii juu ya kwamba inafaa kuwaswalisha mkusanyiko familia nyumbani. Je, utumiaji dalili wake ni sahihi?

Jibu: Inafaa kufanya hivo baadhi ya nyakati. Ni kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtembelea bibi yake Anas na akawaswalisha mkusanyiko. Kwa hivyo akifanya hivo baadhi ya nyakati na mtu akawaswalisha mkusanyiko hapana vibaya.

Swali: Anayeacha swalah ya mkusanyiko ili awaswalishe watoto wake?

Jibu: Haijuzu kufanya hivo. Ni lazima kuswali na mkusanyiko. Kama anataka kuwafunza basi awaswalishe mkusanyiko.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23784/ما-حكم-صلاة-الرجل-النافلة-باهل-بيته-جماعة
  • Imechapishwa: 26/04/2024