Swali: Ikiwa aliyeajiriwa kwa kazi anatumia mshahara ambao unaweza kufikia robo ya mshahara wa mwenzake katika raia wa nchi. Je, hili linajuzu kutoka kwa upande wa taasisi iliyomleta huyu aliyeajiriwa? Je, inajuzu kwa huyo aliyeajiriwa kufanya kazi ya ziada baada ya kukamilisha kazi aliyoletwa kwa ajili yake kwa mshahara unaoweza kumsaidia katika maisha kutokana na udhaifu wa mshahara wake wa msingi, pamoja na wingi wa majukumu yake?
Jibu: Mishahara iko juu ya masharti:
“Waislamu wako juu ya masharti yao.”
Inajuzu kumleta mmoja kwa 1,000 na mwingine kwa 2,000. Si sharti walingane. Watu si sawa katika uzoefu, katika uelewa wala katika uwezo. Wafanyakazi wanatofautiana na waajiriwa wanatofautiana. Wako juu ya yale waliyokubaliwa kuletwa juu yake. Ikiwa aliwaleta juu ya 500 na akawaleta wengine juu ya 1,000, katazo liko wapi? Waislamu wako juu ya masharti yao. Hakuwadhulumu. Wamekuja kwa uchaguzi wao juu ya 500, mwingin ju ya 1,000 na kadhalika. Huenda akawa na wafanyakazi wa aina mbalimbali. Miongoni mwao yupo wa 1,000, mwingine wa 500 na mwingine wa 300. Kwa hiyo hakuna ubaya katika hili. Muhimu ni iwe kwa ridhaa, makubaliano na masharti ya kabla ili asije akaja isipokuwa juu ya uoni wa ndani. Si sharti wawe sawa katika mshahara. Hata waajiriwa wa sasa wa raia hawalingani; huyu ana hiki na huyu ana kile. Kisha watu katika elimu yao, katika sifa zao na katika uwezo wao wanatofautiana. Vivyo hivyo walioajiriwa wanatofautiana katika taarifa zao, katika uwezo wao na katika sifa zao, hawalingani. Tegemeo katika hili ni makubaliano na masharti:
”Waislamu wako juu ya masharti yao.”
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3459/الاجور-على-حسب-الشروط
- Imechapishwa: 31/08/2026
Swali: Ikiwa aliyeajiriwa kwa kazi anatumia mshahara ambao unaweza kufikia robo ya mshahara wa mwenzake katika raia wa nchi. Je, hili linajuzu kutoka kwa upande wa taasisi iliyomleta huyu aliyeajiriwa? Je, inajuzu kwa huyo aliyeajiriwa kufanya kazi ya ziada baada ya kukamilisha kazi aliyoletwa kwa ajili yake kwa mshahara unaoweza kumsaidia katika maisha kutokana na udhaifu wa mshahara wake wa msingi, pamoja na wingi wa majukumu yake?
Jibu: Mishahara iko juu ya masharti:
“Waislamu wako juu ya masharti yao.”
Inajuzu kumleta mmoja kwa 1,000 na mwingine kwa 2,000. Si sharti walingane. Watu si sawa katika uzoefu, katika uelewa wala katika uwezo. Wafanyakazi wanatofautiana na waajiriwa wanatofautiana. Wako juu ya yale waliyokubaliwa kuletwa juu yake. Ikiwa aliwaleta juu ya 500 na akawaleta wengine juu ya 1,000, katazo liko wapi? Waislamu wako juu ya masharti yao. Hakuwadhulumu. Wamekuja kwa uchaguzi wao juu ya 500, mwingin ju ya 1,000 na kadhalika. Huenda akawa na wafanyakazi wa aina mbalimbali. Miongoni mwao yupo wa 1,000, mwingine wa 500 na mwingine wa 300. Kwa hiyo hakuna ubaya katika hili. Muhimu ni iwe kwa ridhaa, makubaliano na masharti ya kabla ili asije akaja isipokuwa juu ya uoni wa ndani. Si sharti wawe sawa katika mshahara. Hata waajiriwa wa sasa wa raia hawalingani; huyu ana hiki na huyu ana kile. Kisha watu katika elimu yao, katika sifa zao na katika uwezo wao wanatofautiana. Vivyo hivyo walioajiriwa wanatofautiana katika taarifa zao, katika uwezo wao na katika sifa zao, hawalingani. Tegemeo katika hili ni makubaliano na masharti:
”Waislamu wako juu ya masharti yao.”
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3459/الاجور-على-حسب-الشروط
Imechapishwa: 31/08/2026
https://firqatunnajia.com/ni-sahihi-mishahari-ya-waajira-kutofautiana-katika-kampuni-moja/