Swali: Mmoja wa ndugu amesema kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anadhulumiwa na akatumia dalili kwa maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

“Hakika shirki ni dhulma kubwa mno!”[1]

Kwa hivyo unapovuka mipaka ya Allaah basi, unakuwa umemdhulumu. Lakini dhuluma inayoendana Naye (Subhaanah). Je, maneno haya ni sahihi?

Jibu: Haifai kusema hivyo. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ

”Hawakutudhulumu Sisi, lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.”[2]

Dhuluma ni kuweka kitu mahali pasipo pake. Haimdhuru Allaah chochote. Bali wao ndio wanaojidhulumu na kubeba athari ya matendo yao. Kwa sababu hii amesema:

وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ

”Hawakutudhulumu Sisi, lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.”[3]

Dhuluma ni kuweka jambo mahali pasipo pake. Maasi ni dhuluma kwa nafsi na utiifu ni faraja kwake. Dhuluma zao na maasi yao havimdhuru Allaah, bali madhara yavyo ni dhidi yao:

إِنْ أَحْسَنتُمْ أَحْسَنتُمْ لِأَنفُسِكُمْ ۖ وَإِنْ أَسَأْتُمْ فَلَهَا

”Mkifanya wema basi mnanjifanyia wema kwa ajili ya nafsi zenu wenyewe, na mkifanya maovu basi ni dhidi yake.”[4]

مَّنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا

”Yeyote atakayetenda mema, basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na yeyote atakayefanya maovu, basi ni dhidi yake.”[5]

[1] 31:13

[2] 02:57

[3] 02:57

[4] 17:07

[5] 41:46

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30983/ما-معنى-قوله-تعالى-ان-الشرك-لظلم-عظيم
  • Imechapishwa: 19/09/2025