Ni pale unapomtaja mwenzako wakati hayuko mbele yako

Swali: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

”Usengenyi ni kumtaja ndugu yako kwa jambo analochukia.”

Je, hili linajumuisha kumsema wakati yupo au wakati hayupo ikiwa hayupo?

Jibu: Hapana, hii ni kumtaja katika hali ya kutokuwepo kwake. Ama akiwa mbele yake, basi hilo ni jambo kati yao wawili. Kwa maana ni kule mtu kumtaja mwenzake kwa mabaya mbele ya watu akiwa hayupo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25214/هل-تقع-الغيبة-في-حق-من-كان-حاضرا
  • Imechapishwa: 22/02/2025