Swalah ni wajibu kwa kila muislamu ambaye kishabaleghe mwanamme na mwanamke.

Kinyume cha muislamu ni kafiri. Kafiri haimlazimu kwake kuswali kwa maana ya kwamba haimlazimu kuitekeleza katika hali ya ukafiri wake wala kuilipa baada ya kusilimu. Lakini ataadhibiwa siku ya Qiyaamah kwa kutokuswali. Allaah (Ta´ala) amesema:

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ

”Nini kilichokuingizeni ndani ya Saqar?” Watasema: ”Hatukuwa miongoni mwa wenye kuswali, na wala hatukuwa tunalisha masikini, na tulikuwa tunatumbukia kwenye upuuzi pamoja na wanaotumbukia upuuzini, na tulikuwa tunaikadhibisha siku ya Malipo.”[1]

Kusema kwao kwamba hawakuwa miongoni mwa waswaliji kunafahamisha kuwa wameadhibiwa kwa kuacha kwao kuswali licha ya ukafiri wao na kuikadhibisha kwao siku ya Malipo.

Ambaye kishabaleghe ni yule ambaye amepata moja katika alama za baleghe. Alama hizo ni tatu kwa mvulana, nne kwa msichana. Nazo ni kama ifuatavyo:

1 – Kukamilisha miaka kumi na tano.

2 – Kutokwa na manii, ni mamoja katika hali ya kuwa macho au katika hali ya kulala.

3 – Kumea nywele sehemu ya siri.

Alama hizi tatu zinakuwa kwa wavulana na wasichana. Wasichana wanakuwa na alama zaidi ya tatu; kupata hedhi.

Kinyume cha mwenye akili ni mwendawazimu asiyekuwa na akili. Miongoni mwao ni mwanamme mzee au mwanamke kikongwe ambaye amefikisha miaka ya kutoweza kuyapambanua mambo, jambo ambalo linatambulika kama mahdhari. Mtu kama huyo halazimiki kuswali kwa sababu ya kukosa akili.

Pia sio wajibu kwa mwenye hedhi kuswali katika kipindi cha ada yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Upungufu wao wa dini ni kule kuacha kwao kufunga na kuswali kipindi cha hedhi yao.”[2]

[1] 74:42-46

[2] al-Bukhaariy (304).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/11-13)
  • Imechapishwa: 23/03/2026