Ni mshirikina kwa mujibu wa wote

Swali: Je, wanazuoni pekee ndio wanaotakiwa kumhukumu mtu kuwa ni mshirikina au watu wa kawaida pia wanapomuona anayeingia ndani ya shirki wanafaa kusema kuwa ni kafiri na mshirikina?

Jibu: Mwenye kudhihirisha shirki ni mshirikina. Mwenye kumwomba asiye Allaah, akamchinjia mwengine asiye Allaah na akaweka nadhiri kwa mwengine asiye Allaah ni mshirikina. Ni mamoja kwa watu wa kawaida na wanazuoni. Mwenye kumwomba ´Aliy na al-Husayn ni mshirikina. Kila mmoja anajua kuwa ni mshirikina.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Durr an-Nadhwiyd (01)
  • Imechapishwa: 06/03/2025