Ni mnyama yupi katika Udhhiyah bora kumchinja?

Swali: Mwaka ulopita nilitaka kuchinja ng´ombe nikaambiwa kwamba kondoo ndio bora. Je, kumethibiti Hadiyth zinazoonesha kwamba kondoo ndio bora zaidi?

Jibu: Ndio. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichinja kondoo wawili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akichinja kondoo na mbuzi. Ikiwa ni wepesi kwake kuchinja kondoo au mbuzi ndio bora. Akichinja vilevile ng´ombe au ngamia hakuna neno. Maswahabah walifanya yote mawili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pia alichinja ng´ombe na ngamia katika hajj ya kuaga kwa ajili ya kujitolea. Kwa hiyo mtu akichinja ngamia au ng´ombe hakuna neno. Lakini kondoo na mbuzi ndio bora kukiwa kuna wepesi wa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/12102/الدليل-على-افضلية-الاضحية-بالكبش
  • Imechapishwa: 17/08/2018