Ni mambo gani yanayowajibisha kuoga?

Swali: Ni mambo gani yanayomlazimisha muislamu kuoga josho? Ni namna gani ya kuoga josho? Je, ni lazima maji yaliyotumika yasilete maji ya awali ya wudhuu´? Ikiwa yamechanganyika nayo, je, inajuzu kukamilisha josho?

Jibu: Miongoni mwa mambo yanayomlazimisha muislamu kuoga josho ni kutokwa na manii wakati wa usingizi, kuingiza kichwa cha dhakari katika tupu hata kama manii hayakutoka, kutokwa na manii akiwa macho kwa sababu ya kupata ladha, hata bila kujamiiana. Pia mwanamke anapopata hedhi au damu ya uzazi, ni wajibu kwake kuoga baada ya damu kukatika.

Ikiwa matone ya maji yaliyotumika yataingia katika maji anayoyaogea, inajuzu kukamilisha josho kwa maji hayo.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/290)
  • Imechapishwa: 12/11/2026