Swali: Nimetawadha kwa ajili ya swalah ambapo nikambeba mtoto na akachafua nguo yangu kwa mkojo. Nikaosha sehemu iliyopatwa na mkojo, kisha nikaswali bila kurudia wudhuu´. Je, swalah yangu ni sahihi?

Jibu: Swalah yako ni sahihi, kwa sababu mkojo wa mtoto uliokupata haukuchengua wudhuu´. Bali ni wajibu kuosha sehemu iliyopatwa na mkojo huo.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/286)
  • Imechapishwa: 12/11/2026