Swali: Ni ipi hukumu ya Kiislamu kuhusu baadhi ya watu wanaovuta sigara, kisha wanapokuja msikitini husukutua vinywa vyao kwa kiasi kidogo cha maji bila kutawadha, wakidai kwamba bado wana wudhuu´? Tunajua kwamba sigara ni miongoni mwa vitu viovu na kwamba vitu viovu vinaharibu wudhuu´, lakini hatuna dalili ya kutosha kuthibitisha kauli hiyo.

Jibu: Kuvuta sigara ni haramu. Mwenye kujaribiwa na uvutaji wa sigara anatakiwa kusafisha mdomo wake anapoelekea msikitini ili kuondoa harufu yake mbaya na kwa kuzingatia kuzuia madhara na kero yake kwa waswaliji. Hata hivyo kuvuta sigara hakuchengui wudhuu´.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/285)
  • Imechapishwa: 12/11/2026