Ni lini mtu huleta Basmalah na Isti´aadhah pindi anaposoma?

Swali: Ni lini mtu huleta Basmalah na Isti´aadhah pindi anaposoma?

Jibu: Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ

“Unapotaka kusoma Qur-aan basi [anza kwa] kuomba kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa.” (16:98)

Ukianza katikati ya Suurah anza kwa kusema “A´udhubi Allaahi minash-Shaytwaani rajiym” kama alivyoamrisha Allaah (Jalla wa ´Alaa).

Kuhusu “Bimillaahi Rahmaani Rahiym” inasemwa ikiwa umeanza kusoma mwanzoni mwa Suurah, kwa kuwa Allaah Ameiteremsha kupambanua baina ya kila Suurah isipokuwa Suurat-ut-Tawbah na al-Anfaal. Hivyo, anza kwa Basmalah mwanzoni mwa kila Suurah. Kuhusiana na Isti´aadhah ilete mwanzoni mwa kila Suurah kabla ya kuanza kusoma na katikati ya Suurah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (43) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-29.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020