Swali 70: Kuna mwanaume anataka kuhiji lakini bado hajaoa, basi ni lipi atangulize?
Jibu: Atangulize ndoa ikiwa anachelea mashaka kwa kuichelewesha. Mfano awe kijana mwenye matamanio makubwa na anachelea juu ya nafsi yake kupata mashaka iwapo ndoa yake itachelewa. Hapa tunaitanguliza ndoa kabla ya Hijjah. Ama ikiwa hali yake ni ya kawaida na haoni ugumu kusubiri, basi atanguliza Hijjah. Hapa ni ikiwa Hijjah hiyo ni ya faradhi. Ama ikiwa ni Hijjah ya kujitolea, basi atanguliza ndoa kwa kila hali, maadamu ana matamanio hata kama haoni ugumu kuichelewesha. Hiyo ni kwa sababu ndoa pamoja na matamanio ni bora kuliko ´ibaadah zinazopendeza, kama walivyosema wazi wanazuoni.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/72)
- Imechapishwa: 26/05/2026
Swali 70: Kuna mwanaume anataka kuhiji lakini bado hajaoa, basi ni lipi atangulize?
Jibu: Atangulize ndoa ikiwa anachelea mashaka kwa kuichelewesha. Mfano awe kijana mwenye matamanio makubwa na anachelea juu ya nafsi yake kupata mashaka iwapo ndoa yake itachelewa. Hapa tunaitanguliza ndoa kabla ya Hijjah. Ama ikiwa hali yake ni ya kawaida na haoni ugumu kusubiri, basi atanguliza Hijjah. Hapa ni ikiwa Hijjah hiyo ni ya faradhi. Ama ikiwa ni Hijjah ya kujitolea, basi atanguliza ndoa kwa kila hali, maadamu ana matamanio hata kama haoni ugumu kuichelewesha. Hiyo ni kwa sababu ndoa pamoja na matamanio ni bora kuliko ´ibaadah zinazopendeza, kama walivyosema wazi wanazuoni.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/72)
Imechapishwa: 26/05/2026
https://firqatunnajia.com/ni-lini-litangulizwe-mwanaume-kati-ya-hajj-na-kuoa/