Bosi kuwapa ruhusa wafanyakazi wanaotaka kwenda kuhiji lakini hawaswali Fajr

Swali 47: Kuhusu mtu ambaye ana wafanyakazi wanaotaka kutekeleza faradhi ya Hajj. Je, awaruhusu hali ya kuwa hawashuhudii swalah ya Fajr?

Jibu: Ikiwa utawaruhusu kwa ajili ya Hajj, basi Allaah akulipe kheri na upewe bishara njema ya badala ya haraka na kwamba kile unachokikosa katika matendo wakati wa Hajj yao, basi Allaah (Ta´ala) atakulipa kilicho bora zaidi kuliko hicho.

Ama kuwa hawaswali swalah ya Fajr, basi wanasihi na watishie kwamba ikiwa hawatahifadhi swalah utawarudisha katika nchi zao. Ni haki kumrudisha yule ambaye hasimamishi swalah katika nchi yake. Kwa sababu hakuna kheri kwa mtu asiyeswali. Ama kuwaruhusu kwa ajili ya Hajj, basi hilo ni wema kutoka kwako. Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akupe ujira.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/56)
  • Imechapishwa: 26/05/2026