Swali: Je, mtu anyanyue kidole cha shahaadah katika kila Dhikr, ni mamoja iwe ndani ya swalah au nje yake, au ni wakati wa du´aa tu?
Jibu: Inapendekezwa kuinua kidole cha shahaadah wakati wa kushuhudia, kuanzia anapokaa mpaka kutoa salamu katika Tashahudi ya mwisho. Vivyo hivyo katika Tashahudi ya mwanzo, aashirie kidole akithibitisha Tawhiyd. Aidha wakati wa du´aa, anakitikisa kidogo anaposema:
اللهم صلِّ على محمدٍ
”Ee Allaah! Mswalie Muhammad!”
Na pale anaposema:
أعوذ بالله من عذاب جهنم
”Najilinda kwa Allaah na adhabu ya Jahannam.”
Na katika du´aa:
اللهم أعني على ذكرك
”Ee Allaah! Nisaidie juu ya kukutaja.”
Katika sehemu za du´aa anakitikisa kidole kidogo, kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Swali: Ni upi usahihi wa mtu kunyanyua kidole cha shahaadah na kutazama mbinguni baada ya kumaliza wudhuu´?
Jibu: Inapendekezwa mtu aseme baada ya kumaliza wudhuu´:
أشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريكَ له، وأشهد أنَّ محمدًا عبده ورسوله، اللهم اجعلني من التَّوابين، واجعلني من المتطهرين، سبحانك اللهم وبحمدك، أشهد أن لا إله إلا أنت، أستغفرك اللهم وأتوب إليك
”Nashuhudia ya kuwa hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah pekee, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Ee Allaah nifanye miongoni mwa wanaotubia, unifanye miongoni mwa waliotwahirika. Umetakasika, ee Allaah na sifa njema zote ni Zako, nashuhudia ya kuwa hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Wewe, nakutaka msamaha, ee Allaah, na ninatubia Kwako.”
Akiashiria kidole cha shahaadah hakuna tatizo. Imepokelewa Hadiyth kuhusu jambo hili, ingawa ina udhaifu. Akikiashiria kwa ajili ya Tawhiyd, hakuna ubaya.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com’
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31697/ما-الاحوال-التي-يشرع-فيها-رفع-السبابة
- Imechapishwa: 12/12/2025
Swali: Je, mtu anyanyue kidole cha shahaadah katika kila Dhikr, ni mamoja iwe ndani ya swalah au nje yake, au ni wakati wa du´aa tu?
Jibu: Inapendekezwa kuinua kidole cha shahaadah wakati wa kushuhudia, kuanzia anapokaa mpaka kutoa salamu katika Tashahudi ya mwisho. Vivyo hivyo katika Tashahudi ya mwanzo, aashirie kidole akithibitisha Tawhiyd. Aidha wakati wa du´aa, anakitikisa kidogo anaposema:
اللهم صلِّ على محمدٍ
”Ee Allaah! Mswalie Muhammad!”
Na pale anaposema:
أعوذ بالله من عذاب جهنم
”Najilinda kwa Allaah na adhabu ya Jahannam.”
Na katika du´aa:
اللهم أعني على ذكرك
”Ee Allaah! Nisaidie juu ya kukutaja.”
Katika sehemu za du´aa anakitikisa kidole kidogo, kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Swali: Ni upi usahihi wa mtu kunyanyua kidole cha shahaadah na kutazama mbinguni baada ya kumaliza wudhuu´?
Jibu: Inapendekezwa mtu aseme baada ya kumaliza wudhuu´:
أشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريكَ له، وأشهد أنَّ محمدًا عبده ورسوله، اللهم اجعلني من التَّوابين، واجعلني من المتطهرين، سبحانك اللهم وبحمدك، أشهد أن لا إله إلا أنت، أستغفرك اللهم وأتوب إليك
”Nashuhudia ya kuwa hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah pekee, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Ee Allaah nifanye miongoni mwa wanaotubia, unifanye miongoni mwa waliotwahirika. Umetakasika, ee Allaah na sifa njema zote ni Zako, nashuhudia ya kuwa hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Wewe, nakutaka msamaha, ee Allaah, na ninatubia Kwako.”
Akiashiria kidole cha shahaadah hakuna tatizo. Imepokelewa Hadiyth kuhusu jambo hili, ingawa ina udhaifu. Akikiashiria kwa ajili ya Tawhiyd, hakuna ubaya.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com’
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31697/ما-الاحوال-التي-يشرع-فيها-رفع-السبابة
Imechapishwa: 12/12/2025
https://firqatunnajia.com/ni-lini-imesuniwa-kuashiria-kidole-cha-shahaadah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket