Ni lini imamu anawageukia waswaliji?

Swali: Ni lini imamu anawageukia waswaliji?

Jibu: Imamu akitoa salamu aseme:

أستغفر الله، أستغفر الله، أستغفر الله، اللهم أنت السلام، ومنك السلام، تباركت يا ذا الجلال والإكرام

”Namuomba Allaah msamaha. Namuomba Allaah msamaha. Namuomba Allaah msamaha. Ee Allaah! Hakika wewe ndiye as-Salaam. Amani inatoka Kwako. umebarikika, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”

Baada ya hapo awaelekee maamuma na alete Tahliylaat hali ya kuwa ameelekea Qiblah. Hivi ndivo imepokelewa katika “as-Swahiyh” ya Muslim kupitia Hadiyth ya al-Mughiyrah, Hadiyth ya ´Aaishah na Hadiyth ya Thawbaan:

أستغفر الله، أستغفر الله

”Namuomba Allaah msamaha. Namuomba Allaah msamaha.”

Hapana neno kuzidisha juu yake. Lakini bora ni atosheke juu yale yaliyopokelewa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 06/11/2021