Ni lazima uwe na kitabu hichi

Miongoni mwa vitabu vingine vilivyopendekezwa ni ”Ta´dhwiym Qadr-is-Swalaah” cha Muhammad bin Naswr al-Marwaziy, ”al-Muntaqaa” cha Ibn-ul-Jaruud, ”al-Musnad” kinachonasibishwa kwa ash-Shaafi´iy, ”al-Bidaayah wan-Nihaayah”, ”at-Tamhiyd” cha Ibn ´Abdil-Barr na tafsiri za Qur-aan za Salaf; tafsiri ya Qur-aan ya Haafidhw Ibn Kathiyr, tafsiri ya Qur-aan ya Ibn Jariyr na tafsiri ya Qur-aan ya al-Baghawiy. Mtu kwa kweli anatakiwa kupatiliza kuwa na tafsiri hizi. Toleo fupifupi hazitoshelezi kutokana na tafsiri ya Qur-aan na Ibn Kathiyr. Unapaswa kutilia umuhimu kuwa na tafsiri ya Qur-aan ya Ibn Kathiry, kwa sabbu ni miongoni mwa vyanzo vikubwa. Wakati fulani akanukuu kutoka katika vitabu ambavyo hivi sasa hatunavyo. Ananukuu kwa cheni za wapokezi, anasahihisha na anadhoofisha. Ni kitabu ambacho mtu anatakiwa kuwa nacho.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 500
  • Imechapishwa: 23/07/2025