Ni lazima Udhhiyah kumgawanya mafungu matatu?

Swali: Kumgawanya mnyama wa Udhhiyah mafungu matatu?

Jibu: Hilo ni chaguo la kikosi cha wanazuoni. Jambo ni jepesi – Allaah akitaka. Amgawanye mafungu matatu, manne au amgawanye wote. Agawanye kile kitachowezekana ijapo kitakuwa kidogo, kwa sababu Allaah amesema:

فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ

“Basi kuleni humo na lisheni ambaye ni fakiri mno.”[1]

[1] 22:28

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/6272/هل-يلزم-تقسيم-الاضحية-على-اثلاث
  • Imechapishwa: 08/06/2024