Swali: Nawachukia ambao hawaswali na wala siwatolei salamu. Je, inafaa kwangu kufanya hivo?

Jibu: Mwenye kuacha swalah akiwa ni mwenye kupinga ulazima wake basi ni kafiri kwa maafikiano ya wanazuoni. Na akiwa ni mwenye kuacha kwa uvivu basi ni kafiri kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao [makafiri] ni swalah. Hivyo basi, yule mwenye kuiacha amekufuru.”

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Baina ya mtu na shirki na ukafiri ni kuacha swalah.”

Ukishayatambua haya basi ni mwenye kutenda dhambi kubwa. Baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa ni kafiri akiiacha ijapo si mwenye kupinga uwajibu wake. Kumsusa mwenye kuacha swalah ni lazima kwa kila muislamu. Ni kama ambavo ni lazima kumkemea na kumtahadharisha mwisho mbaya wa kitendo chake. Ni lazima kwa mtawala kumwambia kutubia. Akitubia ni vyema na venginevyo auliwe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/308)
  • Imechapishwa: 17/09/2021