Ni lazima kwa bosi kuwapa idhini wafanyikazi wakahiji?

Swali: Mimi nina wafanyikazi ambao wanataka kwenda kutekeleza faradhi ya Hajj. Je, niwaruhusu? Wako katika dhimma yangu? Pamoja na kujua ya kwamba hawashuhudii swalah ya Fajr?

Jibu: Ukiwapa idhini ya kwenda kuhiji Allaah akujaze kheri na nakupa bishara njema juu ya yale utayopoteza kipindi wako Hajj basi – Allaah akitaka – atakulipia bora kuliko uliyoyapoteza.

Kuhusu kwamba hawaswali swalah ya Fajr wanasihi na watishe kwamba wasipohifadhi juu ya swalah basi utawarudisha kwenye nchi zao. Ni sawa kufanya hivo kumrudisha yule asiyesimamisha swalah katika nchi yake. Hana kheri huyo. Hakuna kheri kwa mtu asiyeswali.

Ama kuhusu kuwapa idhini wakahiji inahesabika ni wema kutoka kwako. Tunatarajia kutoka kwa Allaah atakulipa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (34) http://binothaimeen.net/content/753
  • Imechapishwa: 29/11/2017