Swali: Ni adhaana ni wajibu kwa anayeswali peke yake? Hadiyth inasema:
“Unaposimama kwa ajili ya swalah, basi tawadha kama alivyokuamrisha Allaah. Kisha shuhudia na ukimu.”[1]
Baadhi ya wanazuoni wanaitumia kama dalili juu ya ulazima wa anayeswali peke yake kutoa adhaana na kukimu. Je, ni sahihi?
Jibu: Ikiwa mtu yuko katika mahali ambapo hakuna waadhini, basi imewekwa katika Shari´ah kwa anayeswali peke yake kutoa adhaana na kukimu, ima kwa njia ya uwajibu au mapendezo. Wanazuoni wamekinzana juu ya hilo. Maoni yote mawili yamesimuliwa kutoka kwa Imaam Ahmad.
Kuhusu ujengeaji wa dalili juu ya Hadiyth iliyotajwa, kuna uwezekano inakusudia shahaadah inayotamkwa baada ya kutawadha – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] at-Tirmidhiy (302).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/161-162)
- Imechapishwa: 06/08/2026
Swali: Ni adhaana ni wajibu kwa anayeswali peke yake? Hadiyth inasema:
“Unaposimama kwa ajili ya swalah, basi tawadha kama alivyokuamrisha Allaah. Kisha shuhudia na ukimu.”[1]
Baadhi ya wanazuoni wanaitumia kama dalili juu ya ulazima wa anayeswali peke yake kutoa adhaana na kukimu. Je, ni sahihi?
Jibu: Ikiwa mtu yuko katika mahali ambapo hakuna waadhini, basi imewekwa katika Shari´ah kwa anayeswali peke yake kutoa adhaana na kukimu, ima kwa njia ya uwajibu au mapendezo. Wanazuoni wamekinzana juu ya hilo. Maoni yote mawili yamesimuliwa kutoka kwa Imaam Ahmad.
Kuhusu ujengeaji wa dalili juu ya Hadiyth iliyotajwa, kuna uwezekano inakusudia shahaadah inayotamkwa baada ya kutawadha – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] at-Tirmidhiy (302).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/161-162)
Imechapishwa: 06/08/2026
https://firqatunnajia.com/ni-lazima-kwa-anayeswali-peke-yake-kutoa-adhaana-na-kukimu/