Ni lazima kwa aliyeingia katika Uislamu kubadili jina lake?

Kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin Baaz kwenda kwa ndugu muheshimiwa H.M.L (Waffaqahu Allaah).

Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh

Wa ba´d:

Jawabu ya barua yako iliyoandikwa tarehe 13-09-1409 H ambapo ndani yake ulikuwa unauliza hukumu ya kubadili jina la mtu ambaye punde ameingia katika Uislamu kutoka katika jina lake la zamani kwenda katika jina la Kiislamu. Je, jambo hilo ni lazima au si lazima?

Jibu: Nakukhabarisha kwamba hakuna katika dalili za Kishari´ah jambo linaloonyesha ulazima wa kubadili jina la ambaye Allaah kamuongoza katika Uislamu. Isipokuwa ikiwa kuna kwa mujibu wa Shari´ah kuna kinachopelekea kufanya hivo. Kwa mfano mtu amejinasibisha kuwa ni mja wa asiyekuwa Allaah kama vile ´Abdul-Masiyh (mja wa al-Masiyh) na mfano wake. Au vilevile ni lazima ambalo si vizuri kuitwa nalo na jina jengine ni bora zaidi kuliko hilo. Kwa mfano Huzn (huzuni) likabadilishwa kwa Sahl (kitu chepesi). Inahusu vilevile majina mengine yote ambayo si vizuri kuitwa kwayo. Lakini kuyabadilisha yale majina yanayoonyesha kuwa mtu ni mja wa asiyekuwa Allaah ni jambo la lazima. Kuhusu majina mengineyo mtu anafanya hivo kwa njia ya mapendekezo na ubora. Yanaingia katika hilo fungu la pili yale majina ambayo imetangaa kwa wakristo kuitwa kwayo na yule mwenye kuyasikia anaingiwa na dhana kwamba mwenye nalo ni mkristo. Kwa hivyo kulibadili ni jambo linalonasibiana kabisa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/153) https://binbaz.org.sa/fatwas/854/%D8%AA%D8%BA%D9%8A%D9%8A%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B3%D9%85-%D8%A8%D8%B9%D8%AF-%D8%A7%D8%B9%D8%AA%D9%86%D8%A7%D9%82-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B3%D9%84%D8%A7%D9%85