Ni lazima kutamka shahaadah wakati wa kuchinja Udhhiyah?

Swali: Tunawasikia watu wakati wa kuchinja wanasema:

باسم الله والله أكبر

“Kwa jina la Allaah, Allaah ni mkubwa.”

lakini hata hivyo hawatamki shahaadah. Je, ni lazima kutamka shahaadah wakati wa kuchinja au si lazima?

Jibu: Sunnah wakati wa kuchinja ni kusema:

باسم الله والله أكبر

“Kwa jina la Allaah, Allaah ni mkubwa.”

Hakuhitajiki shahaadah. Mtu amtaje na kumkabiri Allaah kisha achinje. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anataka kuchinja alikuwa anasema:

باسم الله والله أكبر

“Kwa jina la Allaah, Allaah ni mkubwa.”

Kisha baada ya hapo ndio anachinja. Ikiwa ni Udhhiyah anasema:

اللهم عن فلان بن فلان، أو عن فلانة

“Ee Allaah! Huyu ni kwa ajili ya fulani bin fulani” na kama ni mwanamke pia anamtaja. Vivyo hivyo ´Aqiyqah ambaye anachinja wanapozaliwa mtoto mchanga. Anatakiwa kusema:

اللهم عن ولدي فلان أو بنتي فلانة

“Ee Allaah! Huyu ni kwa ajili ya mwana wangu fulani au msichana wangu fulani.”

Hakuna neno kufanya hivo. Hili ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Lakini ni lazima aseme wakati wa kuchinja:

سم الله والله أكبر

“Kwa jina la Allaah, Allaah ni mkubwa.”

Kisha ndio amchinje au kumtoboa tundu ikiwa Udhhiyah ni ngamia. Ama akiwa ni ng´ombe, kondoo au mbuzi anachinjwa kwa namna yake ambavyo ni rahisi. Hawa wanachinjwa kwa kisu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/10337/%D9%85%D8%A7-%D9%8A%D9%82%D8%A7%D9%84-%D8%B9%D9%86%D8%AF-%D8%B0%D8%A8%D8%AD-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B6%D8%AD%D9%8A%D8%A9-%D9%88%D8%BA%D9%8A%D8%B1%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 15/08/2018