Ni lazima kusugua mwili wakati wa kuoga janaba?

Swali: Pindi mtu anaoga josho la janaba inatosha mtu akamwaga maji juu ya mwili au ni lazima vilevile mtu asugue kwa mkono?

Jibu: Kusugua ni kitu kilichopendekezwa tu na sio jambo la lazima. Lakini ikiwa yuko na kitu mwilini mwake ambacho hakiondiki kwa maji basi anapaswa kukisugua. Muhimu ni kupitisha maji juu ya mwili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 23/05/2021