Swali: Je, ni lazima kwa anayenasihiwa kuzifanyia kazi nasaha?

Jibu: Ikiwa nasaha zinaafikiana na Shari´ah basi ni wajibu kwa mnasihiwa kumcha Allaah na aikubali haki. Vivyo hivyo kuhusu ambaye anaamrishwa mema na kukatazwa maovu analazimika kumcha Allaah na kukubali kile alichonasihiwa muda wa kuwa mnasihi amemsimamishia dalili na haki imemkuia wazi.

Nasaha ni zenye kuenea hata katika mambo ya kilimwengu kama vile udanganyifu katika miamala na mengineyo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Dini ni kupeana nasaha.”

Ni yenye kuenea. Vilevile Jariyr al-Bajaliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Nilikula kiapo kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) cha kusimamisha swalah, kutoa zakaah na kumnasihi kila muislamu.”

Nasaha kuwapa waislamu ni wajibu. Kuhusu makafiri ni wajibu kwanza kuwalingania katika kumwabudu Allaah pekee wakati mtu ana uwezo wa kufanya hivo. Huku ndio kuwanasihi. Unatakiwa kwanza kuwalingania kwa Allaah kabla ya kuingilia mambo mengine. Unapaswa kuanza kulingania kwa Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah (07)
  • Imechapishwa: 05/11/2024