Swali: Je, maandiko ya Aayah yanamaanisha kuwa utoaji wa zakaah unapaswa kufuata mpangilio maalum au mtu anayo khiyari?
Jibu: Dhahiri – na Allaah anajua zaidi – ni kwamba kutajwa kwa makundi katika Qur-aan kunaashiria daraja na umuhimu, kwamba kundi la kwanza ndilo lililo na haki zaidi. Hata hivyo Aayah haina mpangilio wa lazima. Lakini kuanza na kundi la kwanza, bi maana mafakiri, kunafahamisha ya kwamba wao ni muhimu zaidi kuliko wengine. Kama alivyoeleza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika masuala ya ´ibaadah:
”Tunaanza na kile alichoanza nacho Allaah.”
Basi kuanza na kile ambacho Allaah ameanza kukitaja ni bora na kina umuhimu zaidi kuliko vingine. Hata hivyo hapana neno ikiwa mtu ataanza na kundi jingine miongoni mwa makundi ya zakaah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1051/هل-مصارف-الزكاة-على-الترتيب
- Imechapishwa: 23/01/2026
Swali: Je, maandiko ya Aayah yanamaanisha kuwa utoaji wa zakaah unapaswa kufuata mpangilio maalum au mtu anayo khiyari?
Jibu: Dhahiri – na Allaah anajua zaidi – ni kwamba kutajwa kwa makundi katika Qur-aan kunaashiria daraja na umuhimu, kwamba kundi la kwanza ndilo lililo na haki zaidi. Hata hivyo Aayah haina mpangilio wa lazima. Lakini kuanza na kundi la kwanza, bi maana mafakiri, kunafahamisha ya kwamba wao ni muhimu zaidi kuliko wengine. Kama alivyoeleza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika masuala ya ´ibaadah:
”Tunaanza na kile alichoanza nacho Allaah.”
Basi kuanza na kile ambacho Allaah ameanza kukitaja ni bora na kina umuhimu zaidi kuliko vingine. Hata hivyo hapana neno ikiwa mtu ataanza na kundi jingine miongoni mwa makundi ya zakaah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1051/هل-مصارف-الزكاة-على-الترتيب
Imechapishwa: 23/01/2026
https://firqatunnajia.com/ni-lazima-kufuata-mpangilio-wa-wanaostahiki-kupewa-zakaah/