Ni kweli eti ni bora kuchinja Udhhiyah katika siku ya pili ?

Swali: Baadhi ya watu wanachinja Udhhiyah siku ya pili baada ya siku ya ´iyd na hawachinji siku ya kwanza ya kuchinja. Hoja yao ni kwamba hivo ndio Sunnah. Wanadumu katika hali hiyo kuanzia zamani mpaka sasa hawajabadilisha jambo hilo. Je, kitendo hicho kinasihi?

Jibu: Bora ni ile siku ya kwanza ya ´iyd, kisha siku ya pili, kisha siku ya tatu, kisha siku ya nne. Kuharakisha ile siku ya kwanza ya ´iyd ndio bora, siku ya pili ni bora zaidi kuliko siku ya tatu, siku ya tatu ni bora zaidi kuliko siku ya nne. Kufanya maalum siku ya pili ni kosa na ni ujinga. Bali bora katika vichinjwa vya Udhhiyah ni kuharakisha katika ile siku ya kwanza ya ´iyd. Vivyo hivyo vichinjwa vya Hadiy; siku ya kwanza ya ´iyd ndio bora. Akichinja siku ya pili ndio bora kuliko siku ya tatu, akichinja siku ya tatu ndio bora kuliko siku ya nne.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/15734/البدار-بذبح-الاضحية-افضل-من-تاخيرها
  • Imechapishwa: 15/06/2024