Ni kafiri yule mwenye kuacha kutoa zakaah kwa ubakhili na uvivu?

Swali: Je, mtu anaweza kusema kwamba mwenye kuacha kutoa zakaah kwa uvivu anakufuru?

Jibu: Hadiyth zimejulisha kwamba mwenye kuacha kutoa zakaah si kafiri. Kwa ajili hiyo siku ya Qiyaamah ataadhibiwa kwa mali yake, kisha ataonyeshwa njia yake ima kuelekea Peponi au kuelekea Motoni. Lau angekuwa kafiri asingalionyeshwa njia kuelekea Peponi, bali angeonyeshwa njia kuelekea Motoni milele. Hayo ni pale aliposema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna mtu aliye na dhahabu au fedha na asiitolei zakaah isipokuwa siku ya Qiyaamah atapewa sahani za Moto zilizochochewa kwenye Moto wa Jahannam kisha apigwe nazo kwenye mbavu zake, paji lake la uso na kwenye mgongo wake. Kila zinapopoa zinatiwa moto tena kwa siku moja ambayo ni sawa na miaka 50.000 mpaka pale waja watakapohukumiwa. Kisha aone njia yake; ima kuelekea Peponi au kuelekea Motoni.”[1]

Hiyo imefahamisha ya kwamba ni mtenda dhambi na kwamba Allaah ndiye mwenye kuamua nini atamfanya.

[1] Muslim (987).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31055/هل-يحكم-على-تارك-الزكاة-تكاسلا-بالكفر
  • Imechapishwa: 26/09/2025