Ni Ipi Hukumu Ya Wanachuoni Wenye Kuogopa Kukataza Shirki?

Swali: Wanachuoni wanaoishi katika miji ya Kiislamu ambapo wanaona kuabudiwa kwa makaburi lakini pamoja na hivyo wakanyamaza juu ya Tawassul zao kwa asiyekuwa Allaah ni wabaya zaidi kuliko wale wanaoifanyia shere dini?

Jibu: Hapa kuna upambanuzi. Ikiwa wanaitakidi kujuzu kwa hilo wanakufuru. Ikiwa wanawachukulia wepesi na wasiwakataze na wasiyafanye na wala hawayaamini watakuwa wamefanya mapungufu katika kuamrisha mema na kukataza maovu. Ama ikiwa wameacha hayo kwa kuogopa ni kama wale [Maswahabah] waliokuwa Makkah na hawakuweza kukataza maovu kwa kuwaogopa washirikina.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 138
  • Imechapishwa: 20/01/2017