Ni ipi hukumu ya mwenye kufanya liwati duniania na Aakhirah?

Swali:  Ni ipi hukumu ya mwenye kufanya liwati duniania na Aakhirah?

Jibu: Hukumu yake duniani, ikithibiti kuwa amefanya hivo ima kwa kukubali mwenyewe au ubainifu, ni kuwa anauawa[1]. Hii ndio hukumu yake duniani kwa njia ya hadd. Kwa njia ya Dini ni kwamba anakuwa fasiki na ushuhuda wake haukubaliwi. Anakuwa fasiki miongoni mwa mafusaki na mfanya dhambi kubwa miongoni mwa madhambi yenye fedheha kubwa baada ya shirki. Ushuhuda wake haukubaliwi mpaka atubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ama kuhusu Aakhirah, jambo lake liko kwa Allaah. Aakhirah ni katika watu wenye dhambi kubwa ilio chini ya shirki. Isipokuwa ikiwa kama anahalalisha liwati, katika hali hii anakuwa kafiri hata kama yeye mwenyewe hakufanya liwati. Akisema kuwa liwati ni halali, huyu ni kafiri mwenye kuritadi katika Dini ya Uislamu. Aambiwe kutubu la sivyo auawe kwa njia ya kuritadi.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/ni-nani-ana-haki-ya-kusimamisha-adhabu-ya-kishariah-%e2%80%82/

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-1-30.mp3
  • Imechapishwa: 11/08/2020