Ni ipi hukumu ya mjamzito kufanya X-Ray ili kujua jinsia ya mtoto?

Swali: Ni ipi hukumu ya kumfanyia uchunguzi mwanamke mjamzito kwa lengo la kujua jinsia ya mtoto kama ni wa kiume au wa kike kwa kutumia vifaa vya kisasa? Je, jambo hili linapingana na maneno Yake Allaah (Ta´ala):

                    إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ

”Hakika Allaah ana ujuzi wa Saa na anateremsha mvua na anajua yale yaliyomo ndani ya matumbo ya uzazi.”[1]?

Jibu: Hapana, halipingani. Baada ya kuumbika halipingani, kwani Malaika hujulishwa na kuamrishwa kama ni wa kiume au wa kike, kama ni mwenye furaha au mla khasara. Kwa hiyo Malaika hujulishwa. Katika hali hiyo inakuwa si jambo tena la ghaibu, kwa kuwa Allaah tayari amemfahamisha. Vifaa vya kisasa vinaweza kuonyesha mtoto ni wa kiume au wa kike, lakini hili si katika elimu ya ghaibu. Elimu ya ghaibu ipo kabla ya kuumbwa, kabla ya kufanyika umbo.

[1] 31:34

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31017/حكم-الكشف-على-الحمل-لمعرفة-نوع-الجنين
  • Imechapishwa: 28/09/2025