Ni ipi hukumu ya kuzipaka nywele rangi nyeusi?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuzipaka rangi nyeusi nywele?

Jibu: Haijuzu. Haijuzu kuzibadilisha nywele kwa rangi nyeusi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Zibadilisheni mvi hizi na jiepusheni na rangi nyeusi.”

Abu Daawuud amepokea ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Katika mwisho wa zama watakuja watu ambao wanapaka rangi nyeusi kama kifua cha njiwa; hawatohisi harufu ya Pepo.”[1]

Haya ni matishio makali. Haijuzu kupaka nywele rangi nyeusi. Mvi zinabadilsihwa kwa rangi nyingine isiyokuwa nyeusi ikiwemo vilevile hina, katam na zafarani.

[1] al-Albaaniy amesema:

”Ameipokea Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, Ahmad, adh-Dhwiyaa’ al-Maqdisiy katika ”al-Mukhtaarah” na wengine wengi ambao hakuna nafasi ya kuwataja. Mlolongo wa wapokezi wake ni Swahiyh na iko kwa masharti ya al-Bukhaariy na Muslim.” (Ghaayat-ul-Maraam, uk. 70-71)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (82) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-08-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2018