Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka viwiko ardhini wakati mtu amesujudu?
Jibu: Hii limechukizwa na haitakikani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Unaposujudu basi weka mikono yake chini na nyanyua viwiko vyako.”[1]
Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake. Pia amekataza kukalia tumbo la mguu wa kushoto na kuusimamisha unyayo wa mguu wa kulia kama anavofanya mbwa. Sunnah ni kunyanyua viwiko vyake. Ni mamoja akiwa mwanamme au mwanamke. Ni mamoja swalah ni ya faradhi au ya iliyopendekezwa. Ategemee viganja vyake vya mikono wakati wa kusujudu.
[1] Ahmad (18022) na Muslim (494).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/154)
- Imechapishwa: 24/10/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Kuosha tupu ya nyuma na ya mbele wakati wa kujisafisha
Swali: Wakati mtu anapojisafisha kwa maji ni lazima kuosha tupu ya mbele na ya nyuma au inatosha kuosha tupu ya nyuma peke yake? Jibu: Ni lazima kuosha tupu ya nyuma na ya mbele pindi kunapotoka uchafu ambao ni kinyesi na mkojo. Kusipotoka kitu na mtu amechengukwa na wudhuu´ kwa sababu…
In "Kutamba kwa maji na mawe"
07. Ubainifu wa namna Mtume alivokuwa akitawadha
Swali 07: Tunaomba kubainishiwa namna ya kutawadha na kuswali kwa mujibu wa ilivyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na haja kubwa ya jambo hilo[1]? Jibu: Imethibiit kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yanayojulisha ya kwamba mwanzoni mwa wudhuu´ wake basi anaanza kuosha viganja vyake…
In "Ahkaam-ul-Musaafir - Ibn Baaz"
Ni yepi ambayo mwanamke anaweza kumuonyesha mwanamke mwenzie?
Swali: Ni yepi ambayo mwanamke anaweza kumuonyesha mwanamke mwenzie? Jibu: Yale yaliyotajwa katika maneno Yake (Ta´ala): وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ…
In "Mavazi ya mwanamke na wanawake wengine"