Ni ipi hukumu ya kuweka vijiti vya mtende na maua juu ya makaburi?

Swali: Je, inajuzu kuweka vijiti vya mtende na maua juu ya makaburi kwa hoja ya kumpunguzia adhabu aliye ndani ya kaburi ikiwa anaadhibiwa, kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hili halikuwekwa katika Shari´ah, kwa sababu Mtume hakulifanya isipokuwa kwa makaburi mawili ambayo Allaah alimjulisha kuwa wanaadhibiwa. Matokeo yake akaweka juu yao vijiti viwili vya mtende na akasema:

”Huenda watapunguziwa muda wa kuwa havijakauka.”

Ama makaburi mengine hakuweka juu yake chochote (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bali aliweka hilo juu ya makaburi mawili ambayo Allaah alimjulisha kuwa wanaadhibiwa. Asiyekuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawezi kujulishwa adhabu ya waliokwishakufa wala hajui hilo. Basi hilo ni katika mambo ya ghaibu. Watu hawajui hilo mpaka aweke juu yake kijiti. Hivyo haipendezi kuweka kijiti wala mtende, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakufanya hivo juu ya makaburi ya watu wa Baqiy´ wala makaburi ya mashahidi. Lau ingelikuwa ni Sunnah na njia ya kujikurubisha angelifanya hivo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wangelifanya hivo Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30928/ما-حكم-وضع-جريد-النخل-على-القبر
  • Imechapishwa: 13/09/2025