Ni ipi hukumu ya kutumia maji taka yaliyosafishwa?

Swali: Hospitali yetu ina maji taka yaliyosafishwa upya. Tunagusana na maji hayo katika sehemu nyingi kutokana na kumwagilia bustani. Huenda tukaguswa hata na matone yake. Je, maji hayo ni najisi yanayobatilisha wudhuu´? Je, miti inayomwagiliwa kwa maji hayo inajuzu kula matunda yake?

Jibu: Ikiwa maji hayo yamesafishwa kwa kiwango ambacho harufu ya najisi, ladha yake na rangi yake zimeondoka na yakawa maji safi, matamu na salama, basi hakuna tatizo katika hilo. Yanakuwa na hukumu ya twahara. Kinachowapata watu kutokana nayo hakidhuru. Miti inayomwagiliwa nayo haidhuru. Matunda yake hayana tatizo.

Ama ikiwa sivyo; kwa maana ya kwamba athari za najisi bado zipo ndani yake, basi hayatumiki, si kwa miti wala kwa mengineyo. Bali yaondolewe sehemu nyingine isiyowadhuru waislamu. Ikiwa yamesafishwa kwa usafishaji kamili na athari za najisi zikaondoka, si kwa rangi, si kwa ladha, wala harufu, basi himdi zote njema ni za Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30053/ما-حكم-مياه-المجاري-المكررة
  • Imechapishwa: 05/09/2025