Ni ipi hukumu ya kuswali swalah nyingine ya mkusanyiko baada ya kumalizika ya kwanza?

Swali: Ikiwa swalah imeshamalizika na kukaja kundi lingine ambao wote hawajaswali. Je, waanzishe swalah ya mkusanyiko nyingine au waswali mmoja mmoja? Kwa kuwa baadhi ya wanazuoni wamechukia kuanzisha swalah ya mkusanyiko nyingine.

Jibu: Ni wajibu wao ni kuswali kwa pamoja na si kuswali mmoja mmoja. Maoni ya baadhi ya wanazuoni kwamba wasiswali pamoja na kwamba waswali mmoja mmoja ni makosa na si sahihi. Bali ni wajibu waswali kwa pamoja, kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyowaamrisha wale waliokuja baada ya watu kuswali na akasema:

“Ni nani atakayempa swadaqah huyu na akaswali pamoja naye?”

Wafanye hivo ili na yeye aweze kupata swalah ya mkusanyiko. Aidha dalili zote za jumla zinaonyesha ulazima wa swalah ya mkusanyiko na fadhila zake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30133/ما-حكم-اقامة-جماعة-ثانية-بالمسجد-بعد-الاولى
  • Imechapishwa: 13/09/2025