Swali: Kuna mtu ameswali akiwa na suruwali na vesti. Je, swalah yake ni sahihi au imechukizwa tu?
Jibu: Kuswali kwa suruwali, ikiwa ni pana au kwa msemo mwingine inaficha vile viungo visivyotakiwa kuonekana na kadhalika vesti ikiwa inafunika mabega mawili basi swalah ni sahihi. Ama ikiwa haifuniki mabega mawili haitakikani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Asiswali mmoja wenu katika nguo moja na begani mwake hakuna kitu.”
Ni lazima kufunika mabega mawili ikiwa mtu ana uwezo wa kufanya hivo.
Wanachuoni wametofautiana mtu kuswali na huku mabega yake yakiwa wazi; swalah yake inasihi au haisihi? Kuna maoni mawili:
1- Kuna wanachuoni waliosema kuwa haisihi.
2- Wengine wakasema kuwa inasihi pamoja na kuwa mtu anapata dhambi.
Ikiwa vesti hii inafunika mabega mawili hakuna neno. Ikiwa suruwali ni yenye kusitiri hakuna neno pia. Lakini lililo bora ni muislamu aswali kwenye nguo mbili. Hivyo ndivo alivosema ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh):
“Allaah akikunjua kunjukeni.”
Mtu aswali na kanzu pamoja na suruwali. Hili ni kamilifu na lenye kusitiri bora zaidi.
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
- Imechapishwa: 28/01/2018
Swali: Kuna mtu ameswali akiwa na suruwali na vesti. Je, swalah yake ni sahihi au imechukizwa tu?
Jibu: Kuswali kwa suruwali, ikiwa ni pana au kwa msemo mwingine inaficha vile viungo visivyotakiwa kuonekana na kadhalika vesti ikiwa inafunika mabega mawili basi swalah ni sahihi. Ama ikiwa haifuniki mabega mawili haitakikani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Asiswali mmoja wenu katika nguo moja na begani mwake hakuna kitu.”
Ni lazima kufunika mabega mawili ikiwa mtu ana uwezo wa kufanya hivo.
Wanachuoni wametofautiana mtu kuswali na huku mabega yake yakiwa wazi; swalah yake inasihi au haisihi? Kuna maoni mawili:
1- Kuna wanachuoni waliosema kuwa haisihi.
2- Wengine wakasema kuwa inasihi pamoja na kuwa mtu anapata dhambi.
Ikiwa vesti hii inafunika mabega mawili hakuna neno. Ikiwa suruwali ni yenye kusitiri hakuna neno pia. Lakini lililo bora ni muislamu aswali kwenye nguo mbili. Hivyo ndivo alivosema ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh):
“Allaah akikunjua kunjukeni.”
Mtu aswali na kanzu pamoja na suruwali. Hili ni kamilifu na lenye kusitiri bora zaidi.
Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
Imechapishwa: 28/01/2018
https://firqatunnajia.com/ni-ipi-hukumu-ya-kuswali-na-suruwali-na-vesti/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)