Ni ipi hukumu ya kuswali mabega wazi?

Swali 06: Ni ipi hukumu ya kufunika sehemu ya juu ya mwili kama kifua na mabega mawili?

Jibu: Ni jambo la lazima, kama ilivyofahamisha Hadiyth:

“Asiswali mmoja wenu katika nguo moja na hakuna katika bega lake kitu.”[1]

Aweke vazi lake la juu kwenye bega lake au aswali kwenye kanzu. Isipokuwa asipopata basi aswali alivyo.

[1] al-Bukhaariy (359) na Muslim (516).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 32
  • Imechapishwa: 05/08/2018