Ni ipi hukumu ya kuswali kwenye msikiti ulio na kaburi?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali kwenye msikiti ulio na kaburi?

Jibu: Ikiwa msikiti huu umejengwa juu ya kaburi basi kuswali ndani yake ni haramu. Vilevile ni wajibu kuubomoa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwalaani mayahudi na manaswara pale walipoyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa ni mahali pa kuswalia akitahadharisha walichokifanya. Ikiwa msikiti ndio ulitangulia kujengwa kabla ya kuingizwa kaburi, basi ni wajibu kuliondosha kaburi hilo msikitini na kulizika mahali wanapozikwa waislamu wengine. Katika hali hii hakuna neno endapo tutalifukua kaburi hili kwa kuwa limezikwa sehemu ambayo haliruhusiwi kuzikwa. Haijuzu kuwazika wafu msikitini.

Ikiwa msikiti ndio ulitangulia kujengwa kabla ya kuingizwa kaburi, basi kuswali ndani yake ni sahihi kwa sharti kaburi hilo lisiwe upande wa Qiblah na watu wakawa wanaswali kulielekea. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuswali kwa kuyaelekea makaburi. Wasipoweza kulibomoa kaburi hilo basi angalau wabomoe muonekano wa msikiti.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/234-235)
  • Imechapishwa: 04/06/2017