Ni ipi hukumu ya kusoma Qur-aan kwa mtindo wa muziki?

Swali: Ni ipi hukumu ya kusikiliza Qur-aan inayosomwa kwa Tajwiyd na wasomaji mashuhuri huku wakisoma kwa kanuni zinazofanana na muziki?

Jibu: Ikiwa usomaji unakwenda zaidi ya kiwango kinachotakiwa na kuzidisha mpaka unaotakiwa, basi haisikiliziwi. Lakini ikiwa wanasoma kwa Tajwiyd na kwa kanuni zisizokuwa na neno – bila ya kuwepo ala za pumbao – hapana vibaya. Ama kusoma kwa namna inayofanana na hali ya anayesoma kwa muziki bila ya kuzingatia mipaka ya usomaji, haikubaliki. Ni lazima msomaji aheshimu mipaka ya usomaji wa Qur-aan.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30974/ما-حكم-تلاوة-القران-على-قواعد-الموسيقى
  • Imechapishwa: 18/09/2025