Ni ipi hukumu ya kupunguza ndevu?

Swali: Ni ipi hukumu ya kupunguza ndevu?

Jibu: Kupunguza ndevu ni kwenda kinyume na yale aliyoamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) pindi aliposema:

“Zirefusheni ndevu… “

“Ziacheni ndevu… “

“Zifugeni ndevu.”

Yule anayetaka kufuata amri na uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) basi asiguse kitu kutoka katika ndevu. Hakika uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) ilikuwa kutokugusa kitu kutoka katika ndevu zake. Vivyo hivyo ndivyo ulivyokuwa uongofu wa Mitume wengine kabla yake. Hakika sote tumesoma maneno ya Allaah (Ta´ala) pindi Haaruun alipomwambia Muusa:

يَا ابْنَ أُمَّ لَا تَأْخُذْ بِلِحْيَتِي وَلَا بِرَأْسِي

“Ee mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu na wala kichwa changu.” (20:94)

Hii ni dalili inayoonyesha kuwa Haaruun alikuwa na ndevu zinazoweza kushikwa. Huo pia ndio uongofu wa Mtume wa mwisho; Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Hakika ndevu zake zilikuwa nyingi na zilizojazana.

Kwa hivyo yule anayetaka kumfuata kikamilifu na kutekeleza amri yake kikamilifu basi asikate kitu kutoka kwenye ndevu zake. Asikate kitu kutoka katika urefu wake wala upana wake.

Baadhi ya watu pindi ndevu zinapoanza kumea zinakuwa ni zenye kuota huku na kule ambapo wanajiambiza kuwa wazinyoe ili ziweze kuota zote kwa pamoja. Hili si sawa. Akizinyoa anakuwa ameasi amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Jengine anaweza kufa kabla ya hazijaota. Ni wajibu kwake kuziacha kama zilivyo. Zinapotimia kuota na kumea zinakuwa katika muonekano mzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/126)
  • Imechapishwa: 30/06/2017