Swali: Ni ipi hukumu ya kupandikiza nywele ambapo zinachukuliwa nywele kutoka nyuma na kuzipandikiza pale pahali ambapo kumeanza upara?

Jibu: Ndio, inafaa. Anayefanya hivo anafanya hivo kwa ajili ya kurudisha uumbaji asili aliyoumba Allaah (´Azza wa Jall) na kwa ajili ya kuondoa kasoro. Sio kwa lengo la kupamba au kuongeza au kubadilisha maumbile ya Allaah. Kile kisa cha wale mabwana watatu ambapo mmoja wao alikuwa na kipara na akataka Allaah amrudishie nywele zake ambapo Malaika akamgusa na hivyo Allaah akampa nywele nzuri[1].

[1] al-Bukhaariy (3464) na Muslim (2964).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/23-24)
  • Imechapishwa: 24/05/2026