Ni ipi hukumu ya kukata swalah baada ya kujua kuwa maiti ni mtenda madhambi?

Swali: Ni yapi maoni yako kwa anayetoka katika swalah pale atapojua kuwa maiti huyo ni katika wafanya maasi kwa lengo la kuwashtua watu na maasi haya?

Jibu: Mtenda maasi midhali maasi yake hayamtoi katika Uislamu basi ni miongoni mwa watu wenye haki zaidi ya kuswaliwa, kwa kuwa anahitajia du´aa. Hivyo inatakiwa kumswalia na kumuombea du´aa. Haitakikani kutoka na kuacha swalah. Isipokuwa ikiwa kama ni mtu ana umuhimu katika mji na wakati huo huo maiti aliyatangaza madhambi yake na akaona kuwa maslahi yanapelekea yeye kutomswalia. Katika hali hii ni sawa [kutomswalia].

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/155)
  • Imechapishwa: 15/09/2021